Mchezaji wa club ya Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 29 ambaye anachezea Club ya Arsenal kapokea ofa ya kulipwa £300,000 kwa wiki sawa na milioni 700 za kitanzania kutoka vilabu viwili vya nchini China kuitosa club yake ya Arsenal msimu huu.
Kwa tetesi zinazo endelea kwenye majalida mabali mbali ya Ulaya na ulimwnguni kote ni kuhusu winga wa Arsenal ambaye kahusishwa kutolewa ofa ya kulipwa £300000 kwa wiki ili kuachana na club ya Arsenal msimu huu.
Dili hili nono ni tofauti na anavyo lipwa kwa sasa na club yake. Club yake inamlipa £190000 kwa wiki sawa na milioni 400+ za kitanzania. Dili hili limetolewa na vilabu viwili tajiri vya china, Guangzhou Evergande na Shanghai SIPG.
Aubameyang ambaye kwa sasa kabakisha mkataba wa miaka 2 na Club ya Arsenal , kwa mujibu wa jalida la uingereza linaeleza vilabu hivyo vya china viliwahi kumtaka Winga huyo kabla hajajiunaga na club ya Arsenal.
Na kwa sasa vilabu hivi vimeendelea kumumendea winga huyo kwa kumtengea dili nono ambalo pengine linaweza mshawishi kuijunga na moja wapo ya club kati ya vilabu hivyo.
Na cha zaidi bodi ya club ya Arsenal imewahi kuinyo timu hio endapo kama hotoweza kufanya vizuri msimu ujao huenda ikamuuza winga huyo kwa hivyo vilabu vya China .
0 Comments