![]() |
Wachezaji wa timu ya Liverpool wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la UEFA champions League |
Aitha, katka mchezo huu timu ya club ya Liverpool ilianza kwa kujipatia goli lake katika dakika za mwanzo mwanzo mwa mechio hio.
Dakika ya 2 baada ya mpira kuanza Liverpool walijipatia benaliti baada ya mpira uliopigwa na Sadio Mane kuuparaza mkono wa mchezaji wa timu ya Totonham ,Mousa Sissoko ndani ya eneo la kumi na nane na ndipo refa aliweza kuipatia timu ya Liverpool penaliti aliyochezwa na Mohamed Salah na kuiandikia timu yake goli la kwanza ama la kuongoza dakika ya pili baada ya kupiga mkwaju wa peneliti.
Kipindi cha kwanza kimemalizika Liverpool iko mbele kwa bao 1 dhidi ya mpinzani wake Totonham.
Dakika ya 87 ndani ya kipindi cha pili Liverpool iliweza kujipatia tena goli la pili kupitia mchezaji wake alie tokea bechi, Divok Origi kuweza kuiandikia bao la pili na la ushindi timu yake ya Liverpool baada ya wachezaji wa Totonham kuchichanganya wakiokoa kona iliyopigwa kuelekezwa katika lango la timu yao.
Dakika ya 90 mpira uliweza kumaliziaka ikiwa watokeo ni 0-2 na timu ya club ya Liverpool iliweza kutunukiwa taji la ubingwa la kombe ya UEFA Champions League.
Hii ikiwa ni mara ya sita kwa timu ya Liverpool kulibeba kombe hilo toka mwaka 2005 ilipoichapa timu ya AC Millan kwa matuta na kuweza kulibeba kombe hilo.
0 Comments