Club ya Machester city imefanikiwa kutwaa kombe la ligi ya EPL (English premium League) baada ya kuichapa club ya Brighton & Hove Albion 1-4 ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani kwa Brighton & Hove Albion.
Aidha mchezo huo ulipigwa kuanzia majira ya saa kumi na moja ndiyo ulioweza kuamua nani ana beba ndoo kati ya Manchester City na Liverpool, ingawa mashabiki wengi wa liverpool walikuwa wakimuombea Manchester City kudraw ama kushidwa katika mechi yake ya ugenini zidi ya Brighton na wao Washinde mechi yao zidi ya Wolverhampton wanderers ambao ulimalzika kwa livepool kushinda 2-0.
Michezo mingne ilyomalizika katika kufunga ligi kuu ilikuwa Burnley vs Arsenal (1-3), Man U vs Cardiff city(0-2), Tottonham Hotspur vs Everston (2-2), Chalsea vs Leceister City (0-0), Watford Vs West Ham United (1-4) ,Fulham vs Newcastle United (0-4), Crystal palace Vs AFC Bournmouth (5-3), na Southampton Vs Huddersfield (1-1). Hivi ndivyo Ligi kuu ya England ilivyomalizika leo tarehe 12/05/2019.
0 Comments