Je unajua ya kwamba mende ni dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu?
Kama tunavyo fahamu ya kwamba mende ni wadudu tunao ishi nao katika mazingira ya majumbani mwetu, haswa katika maeneo kama vile kabati za vyombo na kabati za nguo, na wengine hupendelea kukaa katika maeneo machafu kama vile chooni na kwenye maeneo ya kutupia taka, au kwa jina jingine majalala (madampo) ya kutupia taka.
Maeneo haya hutumika kama masikani,mazalia na sehemu ya kujipatia chakula cha hawa wadudu.
Lakini kikubwa zaidi ambacho nataka kukujuza ni kuhusu suala la huyu mdudu kutumika kutengenezea dawa za kutibu magonjwa mbalimbali kama vile homa, malaria, maumivu makali ya tumbo na mfumo wa hewa. Hii imeweza kugundulika huko nchi China ambapo kuna mashamba yamenzishwa kwa ajiri ya ufugaji mende.
Aidha mashamba hayo yanauwezo wa kuzalisha mende zaidi ya bilioni sita na kuweza kuchangia pato la taifa kwa kuingiza Yuan bilioni 4 na zaidi.
Inadaiwa kuwa mdudu huyu anauwezo wa kuishi muda mrefu na kingine ambacho ulikuwa hujuwi , kutoka na utafiti wa kisayansi inasemekana mdudu huyu hata akitolewa kichwa anauwezo wa kuendelea kuishi kutokana na sehemu ya ubongo wake kupatikana sehemu ya mwili wake yaani tumboni tofauti na ilivyo kwa wadudu na wanyama wengine.
0 Comments