Lesotho imefanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" bao 1 kwa 0 kwenye mchuano huo uliopigwa katika nchi ya Lesotho huko kusini mwa Afrika. Katika dakika ya 76 ya mchezo huo Lesotho iliweza kujipatia bao moja ambalo lilidumu mpaka mchezo unamalizika na kuiwezesha Lesotho kubeba alama 3 za mchezo.
Kwa sasa katika kundi la timu hizi linaongozwa na UGANDA ikiwa na jumla ya alama 10 ikifatiwa na TANZANIA ambayo inajumla ya alama 5, CAP VADE ikiwa na jumla ya alama 4 pia LESOTHO ikiwa na alama 4.
0 Comments